Baptism

Mathayo 28:19-20.Basi,enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa   jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu;Nakuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi;na tazama nipo pamoja nayi siku zote;hata ukamilifu wa dahari.

WOTE NI WATENDA DHAMBI,WOTE TUNAHITAJI KUAMINI.

Kwa muda wa miaka mingi giza la mpinga Kristo limekuwa linadangaya wakristo Ulaya.Upapa uliweka mafundisho ya wanadamu katika andiko.Mungu aliwainua watu wamatengenezo kuleta ukweli wa neno la Mungu kwa watu.Watu hawa waliyachunguza maandiko na Mungu alifunua ukweli kwao.Upapa ulifundisha kuwa kuna sakramenti saba.Baadhi ya waprotestanti wanazikana zote saba wakianguka kuchukua maelezo ya kile ambacho Biblia inafundisha.Wanamatengenezo ya Kilutheri kwa umakini wamejifunza neno la Mungu na kuona kwa uwazi sakramenti mbili.Ubatizo na meza ya Bwana.Neno huonyesha kile tunachokiita sakramenti kama matendo matakatifu yaliyoanzishwa na Kristo.Akitumia neno la Mungu,kwa kuvijumuisha vitu vya kidunia ambavyo huleta msamaha wa dhambi.Wanamatengenezo wa Kilutheri waliepuka mawazo ya kipapa ambayo yakuongezeka kwenye neno la Mungu na pia waliepuka wazo jingine la kupunguza kutoka katika neno la Mungu na wakiacha mawazo ya kibinadamu kutawala maandiko.Ubatizo ni mojawapo ya sakramenti hizo mbili.

UBATIZO HUFANYA NINI?

Katika agizo kuu la Bwana wetu kama ilivyonukuliwa katika Mathayo sura ya 28, anatuambia kufanya wanafunzi Mataifa yote.Kufuatilia agizo la kufanya wanafunzi .Alitumia wakati uliopo, hali ya kuendelea.Hali ya kuendelea ni kubatiza na kufundisha.Kwa hili hutuambia jinsi yakufanya wanafunzi, nayo nikubatiza na kufundisha.Tunaamini nakulitendea kazi hili kama kanisa la mwanzo la Kimitume lilivyofanya.

Kwa watu wazima tunafundisha na kubatiza.Kwa watoto tunabatiza nakufundisha.Katika namna yake neno la Mungu lina nguvu zote kufanya wanafunzi wakati tunapowabatiza watoto, Roho mtakatifu huumba imani katika moyo kwa utendaji wa jina la Mungu wa utatu “Kwa jina la Mungu Baba,na la mwana na Roho mtakatifu”Kubatiza katika jina lake hutupa kuingia katika familia ya Mungu.

Kwa watu wazima tunafundisha nakubatiza.Ni neno la injili lenye nguvu zote ambalo huumba imani katika moyo wa mtu mzima sawasawa na mtoto mchanga.Wakati mtu mzima anapotangaza imani katika Kristo tunambatiza.Hili linatia nguvu imani.Hufanya kazi sambamba kama sakramenti ya madhabahu au injili katika neno.Tunafundisha na kubatiza watu wazima kwa sababu wanaweza kuelewa lugha.

Kwa watoto tunabatiza na kufundisha, tangu wanapoanza kuelewa lugha na kukiri kwa midomo yao.Wazazi wakristo huleta watoto wao katika ubatizo kwa ujasiri wa kuumba nguvu ya neno na kwa agizo la Yesu.Mtoto baadaye anaweza kukataa ubatizo wake,hili ni kweli.Lakini ni jukumu la wazazi kuwalea watoto wao katika malezi na kumcha Mungu(Waefeso 6:4 Nanyi wakina baba, msiwachokoze watoto wenu ;bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana).

 

KWA NINI UBATIZO UMEKUSUDIWA?

Fundisho letu ni sawa na lile lililofundishwa na Mitume.Kiasili tunategemea fundisho la Kimitume,ili kueleza kuwa ubatizo umekusudiwa kwa nani.Kwanza ya vyote tunaona katika agizo kuu lililoandikwa katika Mathayo kwamba  “mataifa yote”yanapaswa kubatizwa.Hili linajumuisha kipindi.Hatuwezi kuondoa watoto wadogo katika “mataifa yote”.Hakuna mpaka uliyowekwa kutoka katika maandiko kwamba watoto hawapaswi kubatizwa.Ni sababu za kibinadamu tuu zinazouliza “umri wa kuwajibika”au umri wa sababu na busara “.Ingawa Petro siku ya Pentecoste alisema kwamba ahadi ni kwa ajili yenu na watoto wenu.Na katika siku ile roho 3000 zikabatizwa,siyo watu elfu tatu waliokuwa na umri wa kuwajibika ,wote wanawajibika kwa Mungu kwa ajili ya dhambi zao za asili kutoka katika kutungwa mimba(Zaburi 51:5)

 

Yesu akasema watoto wadogo waje kwake na mtu yeyote asiwazuie.Mathayo 19:14.Alitumia neno  “watoto wadogo”Hapa Bwana wetu anaelekeza kwamba watoto wanahitaji wokovu kutoka katika kutungwa mimba.Jinsi gani wanaweza kuokolewa?siyo kwa kupitia imani ya wazazi wao,kwa sababu hakuna mtu anaweza kuokoa ndugu yake.Siyo kwa sababu hawapo na hatia na si watenda dhambi,kwa sababu ni wenye dhambi kwa asili.Mungu ametupatia ubatizo.Tunajifunza kwamba katika safari ya pili kule Filipi,alimbatizwa mlinzi wa gereza pamoja na familia yake(Mdo 16:33)na Lidia pamoja na nyumba yake(Mdo 16:15)zinapingana na fikra za kawaida za neno kutojumuisha watoto.

IKO WAPI  NGUVU YA UBATIZO?

Tunawafundisha watoto katika kateksimo,jinsi gain ya maji yanaweza mambo haya makubwa?.Siyo maji hasa yanafanya hayo lakini ni neno la MunguAmbalo lipo ndani ya maji,na imani ambayo huamini hili neno la Mungu katika maji.Kwa maana bila neno la Mungu maji ni kama maji ya kawaida na hakuna ubatizo.Lakini pamoja na neno la Mungu ni ubatizo,hayo ni maji ya neema ,ya uhai na kuoshwa kwa wanyoofu katika Roho Mtakatifu.Paulo katika kumwandikia Tito hueleza nguvu ya ubatizo (Tito 3:5 Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi;bali ni kwa rehema yake,kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.Bwana wetu alimwambia Nikodemu kwamba anapaswa kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa neno.Huu ni ufufuo/wongofu katika kifungu cha Tito.

Petro pia kwa udhahiri hueleza nguvu ya ubatizo “ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi;(siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili,bali ni jibu la dhamiri safi mbele za Mungu)kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. (1Pet 3:21).Nguvu ya ubatizo ipo katika neno la Mungu lililotumika. Na hii ni nguvu iokoayo.Si zaidi sherehe ya nje bali kazi itendekayo ndani ya moyo,kufanywa upya katika Roho Mtakatifu.Ubatizo ni nguvu ya kutusukuma kwa Kristo “Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake,kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba,vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

NAMNA GANI YAKUBATIZA?

Ni wazi kwamba ubatizo lazima uwe katika jina la Mungu wa utatu kama tulivyoona katika Mathayo 28.Kubatizwa katika jina la Kristo humaanisha kwa jina la Mungu wa utatu,kama ilivyoamuriwa.Kama vile ambayo hakuna makubaliano kati ya Protestanti juu ya ubatizo wa watoto wadogo,hivyo pia  kuwa pia na kutokukubaliana na jinsi ya kutumia maji katika ubatizo.Katika sehemu zote tatizo huibuka kwa sababu baadhi kiurahisi hawataki kuwa wanafunzi wa andiko.Ingawa huchagua kufuata miongozo ya sababu ya kibinadamu.Bwana Yesu hakuweka wazi jinsi gani maji yangepaswa kutumika.Lakini aliamuru kwamba maji yatumike.Kwa ujumla kuna aina tatu za kubatiza kwa wakristo, “Kunyunyiza,kumwagiwa na kuzamishwa”.

Kuna hao wanaosema ni lazima uzamishwe ndani ya maji au itakuwa  haujabatizwa kiuhalali,wanafanya makosa kwa kutofikiri juu ya neno(batizo) kama vile lilivyotumika katika Agano jipya.Kama lilikuwa ni (bapto)hivyo lingekuwa bora zaidi kuzamisha au kuchovyo.Lakini neno siyo(bapto) lakini baptizo ambalo lilitumika katika Agano jipya katika fikra ya kuosha katika kutia maji.Katika Mariko 7:2-5,Luka 11:38 na Waebrania 9:10.Btiza lilituimiwa katika fikra za sherehe za Kiyahudi kutawadha/kuosha.Na wakati tunapofikiri juu ya ubatizo wa Roho mtakatifu siku ya Pentekoste alimwagwa (Mathayo 3:11,Mdo 2:16-17).

Andiko huturuhusu kutumia maji katika njia tofauti.Tungepaswa kufundisha yote  ambayo Biblia hufundisha,na wala sio kuongeza ndani yake, na wala sio kuondoa ndani yake. Kwa mfano, namna ya kunyunyiza maji ni nzuri yaleta kukumbuka jinsi gani katika Patakatifu pa  Patakatifu katika siku ya upatanisho,damu ilinyunyizwa kwa ajili ya kusafisha dhambi.Mwandishi wa kitabu cha Waebrania hutumia alama hiyo, “Waebr 10:22” nafikiri kwamba   Ezekieli anarejea katika ubatizo kwa kutumia alama kutoka katika upatanisho, “Ezek 36:25-26

Njia nyingine ya kubatiza kwa maji ni kumwagiwa. Hii inatukumbusha siku ya Pentekoste wakati Roho Mtakatifu alipomwagwa juu ya wanafunzi. Kwa maji na kwa Neno huja Roho Mtakatifu. Tunafikiri pia na tumaini halitahayari kwa maana pendo la MUNGU limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. “Warumi 5:5”

Kuzamishwa ni namna nyingine ya ubatizo. Sisi pia tunatumia ufafanuzi huu katika Katekisimo yetu,“Kubatizwa kwa maji huku kunamaanisha nini? Kuna maanisha kwamba Adamu wa kale ndani yetu ni kuzamishwa  kwa kitubio cha kila siku na toba,na ni kufa kwa dhambi na tamaa mbaya;tena mtu mpya hupaswa kila siku kuja mbele na kuinua ambaye anaishi mbele za Mungu katika Haki na Utakatifu milele”

Njia halisi  ya kutumia maji siyo ya muhimu ukilinganisha na ukweli wa tendo halisi la kubatizwa, “Aaminiye na kubatizwa ataokoka,bali asiyeamini atahukumiwa” Marko 16:16.

HITIMISHO

Ubatizo ni kazi ya Mungu kupitia nguvu ya Neno lake juu ya uumbaji wa Moyo na kuimarisha imani. Lakini Ubatizo bila kuendelea katika Neno lake inamaanisha kupoteza Msamaha uliotolewa wa kuoshwa kwa uongofu. Ubatizo bila kuendelea katika Neno ni kama kupanda mti katika Jangwa. Bila kuumwagilia mti utakufa.Ni lazima kuendelea kuwa na maji safi ya neno linalotujia ndani yetu,“Chemichemi ya maji yakibubujika uzima wa milele (Yohana 4:14)”.